Serikali inatarajia kuweka na sheria kali dhidi ya wanaofanya ukatili wa kijinsia kwenye jamii ili kuondoa na kupungunguza wimbi la ukatili linaloendelea kwenye jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa majibu yap apo kwa papo kwa Waziri Mkuu akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Tunza Malapo aliyeitaka serikali kupeleka Muswada bungeni wa kuongeza adhabu ama kubadili adhabu zitakazokidhi ili kuondoa matukio hayo.
Akijibu swali hilo Waziri mkuu amesema “kwakuwa nimekiri tatizo hilo lipo kwenye lamii kwa baadhi ya maeneo nah atua kali zinachukuliwa na inawezekana yanajirudia kwa baadhi ya maeneo ambayo yanasheria ambazo sheria zake si kali sana kwasababu jambo hili ni mtambuka linaguza wizara nyingi na kila wizara inaweka sheria yake katika kukinga jambo hili tunapokea ushauri wa kufanya mapitio ya sheria hizi malengo yetu nu kuhakikisha jamii inabaki kuwa salama na wale wote wanaotenda matendi yote ya ukatili wa kijinsia waendelee kuchukuliwa hatua kali na tunatamani jambo hili lionekane linakoma katika jamii” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa