Beki wa Barcelona Ronald Araújo anasema kuwa atajadili mustakabali wake katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Araújo, 25, ana mkataba na Barca hadi Juni 2026 na amekuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo ili kuongeza mkataba wake. Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay anaripotiwa kulengwa na Bayern Munich na Manchester United.
“Mkataba wangu mpya uko kwenye mkondo mzuri, lakini tutakaa chini kwa mazungumzo sahihi mara tu msimu utakapomalizika,” Araujo alisema. “Nina furaha sana kuwa Barcelona, familia yangu ina furaha, nitatoa kila kitu hadi mwisho.”
Siku ya Alhamisi, Araújo alikataa kujibu ukosoaji wa mchezaji mwenzake Ilkay Gündogan kuhusu kutolewa kwake kwa kadi nyekundu dhidi ya Paris Saint-Germain.
Gündogan alikasirishwa na kadi nyekundu ya Araújo dakika ya 29 wakati Barca ilipopoteza 4-1 dhidi ya PSG katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumatano, akisema ilisababisha timu yake kufa. Na Akizungumza katika hafla ya kutoa misaada huko Barcelona, Araújo alijibu: “Napendelea kuweka kwangu kile ninachofikiria kuhusu maoni ya Gündogan. Nina maadili fulani na yanapaswa kuheshimiwa.”