Imeelezwa kuwa wanawake kati ya 10 wanaofanyiwa Vipimo vya Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi watatu hugundulika na Ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Mlango wa Kizazi ndani ya Mkoa wa Geita .
Akizungumza na Wandishi wa habari Mratibu wa huduma za Chanjo Mkoa wa Geita Bi. Wile Ruhangija amesema serikali imeleta Chanjo ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa mkoa wa Geita kwa watoto walio chini ya umri kuanzia miaka 9 mpaka 14.
“Chanjo hii itatolewa katika Mkoa wetu kuanzia tarehe 22 mwezi wa nne mpaka tarehe 28 lengo kuu ni kuwakinga mabinti wenye umri wa miaka 9 hadi 14 dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi katika Mkoa wetu wa Geita tunalo lengo la watoto laki 2 na 76436 ambao tutawafikia kuwakinga na saratani ya Mlango wa kizazi , ” Mratibu wa huduma za Chanjo Mkoa wa Geita.
Bi.Luangija amesema kwa mkoa wa Geita wanatarajia kuchanja watoto wa kike Laki 2 na 76 Elfu na 436 huku akiwataka wazazi na walezi kuwaleta watoto wao katika vituo kupata chanjo hiyo.
Mwakilishi kutoka wizara ya Afya Dkt. Marwa Mwikwabe amewaondoa hofu wale wote ambao wamekuwa na imani potofu kupitia chanjo hizo huku akiwataka wananchi kuwaleta watoto wao kwani chanjo zimethibitishwa na shirika la Afya ulimwenguni (WHO) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini.
“Lengo hasa kitaifa tunatakiwa kuchanja jumla ya wasichana ambao wanaumri kati ya Miaka 9 mpaka 14 lengo ni kuchanja milioni 5 elfu 28 na 357 hao ni jumla ya nchi nzima lakini kwa Tanzania bara tunatarajia kuchanja jumla ya wasichana milioni 4 laki 8 na 41 elfu 298 , ” Mwakilishi wizara ya Afya Dr Marwa.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Dkt. Stephen Mwaisobwa amewataka wazazi na walezi kuwaleta watoto wao wakike pamoja na wazazi wa kike kuwa na mazoea ya kufanya vipimo hasa zinapokuwa zinakuja chanjo hizi katika maeneo yao.