Vijana wametakiwa kutumia elimu zao katika kujiendeleza na kubuni miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato kwani serikali inatoa mikopo kwa vijana hivyo ni fursa kwao kuchangamkia mikopo hiyo.
Akizungumza katika bonanza la michezo lilo andaliwa na chuo cha masai utalii college na kuhusisha wana michezo kutoka vyuo mbalimbali ndani ya jiji la Tanga katibu tawala wa wilaya ya Tanga ambaye alikuwa mgeni rasim kwenye bonanza hilo Dalim Mikaya alisema ni wakati sasa kwa vijana kutumia elimu zao katika kubuni miradi mbalimbali itakayo waingizia kipato nahivyo kujikwamua na wimbi la ukosefu wa ajira.
“Rais wetu amerudisha tena mikopo kwa vijana na dhani mnafahamu hilo hivyo niwasihi vijana wenzangu kuchangamkia fursa katika kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kuomba mikopo hiyo ambayo itawasaidia katika kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira na hivyo itawasaidia kupata kipato”
Aidha dalimia alisema kuwa michezo inaunganisha vijana Pamoja,hivyo amewataka vijana hao kutumia michezo hiyo kama njia moja wapo ya kuwaepusha na matendo maovu kama matumizi ya madawa ya kulevya na sambamba na kuimarisha miili yao dhidi ya magonjwa .
Kwaupande mkuu wa chuo cha masai utaliii college Rosedarlen Hilary alisema kuwa lengo la bonza hilo ni kutoa elimu kwa vijana juu ya uchaguzi,teknolojia,afya ya akili,matumizi ya madawa ya kulevya Pamoja na afya ya uzazi ili kuwajengea uelewa vijana kuweza kujitambua,sambamba na hayo vijana hao wameshiriki katika kufanya usafi katika kituo cha afya makorora na kutoa vitu mbalimbali kwa wodi ya wakina mama wajawazito.
Aidha baadhi ya washiriki wa bonza hilo wamewaomba wadau wa michezo kutembelea mabonza mbalimbali yanayo fanywa na vyuo ili kuweza kuibua vibaji vitakavyo tumika kwenye timu zetu za taifa.
“niwakati sasa kwa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini kuweka kipaombele kwenye timu zetu zinazo shiriki ligi mbalimbali kuwa na wachezaji wengi wa ndani kwa kufanya hivyo kutawezesha vijana wengi hapa nchini kuonesha uwezo wao kwenye timu hizo na hivyo kuwa na faida kwenye timu ya taifa”