Mkuu wa wilaya ya Geita Hashimu Komba amempiga Marufuku Afisa Mfawidhi LATRA Mkoa wa Geita Bw.Rajabu Selemani kwa tabia ya kukamata Pikipiki na Bajaji na kwenda kuzifungia katika eneo linalofahamika kama Coka kwa lengo la kujipatia kipato cha Shilingi 5000 kwa siku hadi pale Mhusika atakapo kuja kukomboa chombo hicho.
Ametoa agizo hilo katika Mkutano Maalumu uliowakutanisha waendesha Pikipiki na Bajaji Mjini humo ambapo Mh.Komba amemuagiza Katibu tawala wilaya ya Geita kushirikiana na Afisa Mfawidhi LATRA kutafta eneo ambalo litakuwa likitumika kuhifadhi Bajaji pamoja na pikipiki na sio kuwatoza tozo ambazo hazipo kisheria.
” Bodaboda na Bajaji ni fursa haiwezi ikawa ni fursa alafu watu wachache wakaanzisha Matozo yanayoumiza Vijana wa Boda boda ninaagiza ninaagiza Mambo mawili yafuatayo jambo la kwanza sisi kama serikali ndani ya Halmashauri ya Mji Geita yako maeneo mengi ya umma ambayo watu wa LATRA na nyinyi ni serikali mnaweza mkafanya mazungumzo kuna eneo pale ambalo lilikuwa linatumika kama halmashauri ya Mji wa Geita kuna iyadi kubwa ipo wazi mnaweza mkaitumia kama iyadi ya kwenu na sio eneo la Mtu binafsi , ” DC. Komba.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi LATRA Mkoa wa Geita Rajabu Seleman amekiri kuwatoza waendesha Bajaji na Pikipiki ambao wamekuwa wakishindwa kulipa faini wanapokutwa na makosa na Vyombo vyao kupelekwa katika eneo la Mtu binafsi linalolindwa ambapo kila chombo ambacho kimekuwa kikilala mule kwa siku kimekuwa kikitozwa kiasi cha shilingi 5000 bila listi ya Malipo.
” Ni kweli suala hilo lipo tunakamata Bajaji ambazo wameshindwa kulipia kwa wakati tulikuwa tunazikamata tunakaa nazo mpaka Jioni siyeweza kulipia analipia anayeshindwa kulipia tulikuwa tunampeleka iyadi kule koka ni kweli ni shilingi 5000 kila akitoka pale anapewa lisiti elfu tano kwa muda gani kwa muda wa siku moja pesa analipwa nani ? Analipwa koka na listi anapewa , ” Afisa Mfawidhi LATRA mkoa wa Geita.
Sakata hilo limeibuka Baada ya Mkuu wa wilaya kufanya Mkutano na Waendesha Bajaji na Pikipiki ndani ya wilaya ya Geita lengo likiwa ni kuona namna ya kupunguza vitendo vya kamata kamata ndani ya wilaya hiyo ndipo ilipoobuka hoja ya kumtuhumu Afisa Mfawidhi LATRA mkoa wa Geita kutoza Kiasi cha Shilingi 5000.