Maofisa na Askari wa Idara ya Uhamiaji kutoka ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Naibu Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth William Mzimiya wametembelea makao ya kulea Wazee ya Nunge Kigamboni ambapo wamewapatia mahitaji muhimu.
Akikabidhi mahitaji hayo Afande Elizabeth alisema, katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam wametoa mkono wa faraja kwa wazee hao wa Nunge lengo watambue kuwa ni sehemu ya jamii ya watanzania na kuwafanya kuwa na amani kwani hao wanahistoria kubwa juu ya Muungano wetu na kutaka wajisikie kuwa wako pamoja nao.
Makao hayo ya kulea Wazee ya Nunge Kigamboni, Jijini Dar es Salaam kwa sasa kina jumla ya Wazee 20 ambapo Wanawake 11 na Wanaume 9 huku kikiwa chini ya Usimamizi wa Serikali kupitia Wizara ya Afya.