Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema kumekuwepo na watu wanaosema yeye ni mpigaji kwa kuamini kwamba anawanyang’anya watu ardhi zao halafu baadae anajimilikisha yeye jambo ambalo amesema ni majungu yenye mlengo wa kisiasa ya watanzania wayapuuze.
Waziri Silaa ametoa kauli hiyo akimaanisha hatorudishwa nyuma na watu wanaopika majungu kuhusu utendaji kazi wake kwamba anajinufaisha na viwanja anavyonyang’anya matapeli na kuwasaidia wananchi.
Ameyasema hayo mkoani Tanga wakati akiagiza wananchi wanyonge waliovunjiwa nyumba zao katika kiwanja na. 4 kilichopo Tanga mjini na tajiri mmiliki wa mabasi ya Tahmed kwa kudai ameshinda kesi kiwanja namba 1.
Aidha, amewaagiza makamisha wasaidizi wote wa ardhi nchini kuandika taarifa za ziara na kazi zake za clinic na kuziwasilisha Serikalini ili wote wanaopelekewa majungu wajiridhishe.
Wakati huo huo tajiri huyo ameingia kwenye mgogoro na Bakwata wamiliki wa Islamic school akidai eneo la kiwanja na.1 alilonunua linafika shuleni.