Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Bi. Grace Kingalame ameungana na viongozi wa Dini na Mila katika kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Taifa Kwa ujumla huku akiwataka wananchi kuendelea kuliombea Taifa.
Akizungumza katika Maombezi hayo DC.Kingalame amesema katika Sekta ya Nishati kwenye wilaya yake vijiji vipatavyo 62 vyote vina umeme na vitongoji 273 kati yao 88 tayari vimefikiwa na huduma hiyo ya Umeme na vina umeme katika wilaya ya Nyang’hwale.
” Tunayo kila sababu ya kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan lakini pia niwaombe viongozi wangu wa Dini msichoke Kumuombea Mwanamke huyu anayefanya kazi usiku na Mchana bila kuchoka anayetamani Maendeleo makubwa katika Taifa letu lakini pia katika wilaya yetu ya Nyang’hwale , ” DC. Kingalame.
Kingalame ameendelea kusema uchumi wa Tanzania bara na Zanzibar umeendelea kuimarika ambapo barabara , Maji Afya na elimu zimeimarika lwa kiwango kikubwa huku akisema katika wilaya hiyo wamebahatika kuwa na shule za Msingi 74 shule za Sekondari 17 vituo vya Afya 4 na Zahanati 32.
Aidha Kingalame amewataka wananchi wa wilaya ya Nyang’hwale kuendelea kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kuendelea kuliombea taifa la Tanzania kwa ujumla.
Baadhi ya viongozi wa Dini kutoka Madhehebu mbalimbali wilayani humo wamempongeza Rais wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika kutambua viongozi hao huku wakisisitiza amani kuendelea kutawala kupitia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioimarishwa tanu mwaka 1964.
Mmoja wa Machief kutoka Himaya ya Msalala wilayani Nyangh”wale Chief Mashauri Omary amekumbushia juu ya umhimu wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar huku akiwaomba wananchi kuendeleza Amani tuliyo nayo.