Inakadiriwa kuwa watu milioni 2.7, wakiwemo wanawake na watoto milioni 1.6, wanaishi katika maeneo ambayo wanadhibiti kikamilifu,” .
Pia alisema Umoja wa Mataifa umethibitisha zaidi ya ukiukwaji wa haki 400 dhidi ya watoto nchini Haiti, na kufichua kuwa zaidi ya watoto 180,000 sasa ni wakimbizi wa ndani.
Mkurugenzi mtendaji alitoa wito wa kuongezwa msaada wa kikanda na kimataifa kwa taifa.
“Lakini hata kama hatua zote zinazofaa zitachukuliwa kumaliza mgogoro huu, hautatatuliwa haraka. Ni lazima tutoe usaidizi wa kina wa kisiasa na kifedha, sasa na kwa muda mrefu,” aliongeza.
Mgogoro wa kisiasa na kuongezeka kwa ghasia za magenge nchini kuliongezeka baada ya mauaji ya Rais Jovenel Moise mnamo 2021.
Maelfu wameuawa katika vita hivyo, huku mamia ya maelfu wakikimbia nchi.