Arsenal na Manchester City wana nia ya kumsajili kiungo wa Newcastle United Bruno Guimarães, kwa mujibu wa Daily Telegraph.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anafahamu nia yake, na kuna kipengele cha kutolewa kwenye mkataba wa kiungo huyo ambacho kitaendelea hadi msimu wa joto wa 2028 ambacho kinamruhusu kusajiliwa kwa ada ya pauni milioni 100.
Newcastle wanaweza kuwa tayari kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kwa ada ya chini huku wakipigania kusalia sawa na kanuni za faida na uendelevu za Premier League.
Guimarães amekuwa katika kiwango cha kuvutia kwa Magpies msimu huu, akiwa amechangia mabao 10 katika mechi 31, na hivi karibuni pia amekuwa akihusishwa na Paris Saint-Germain.
Hata hivyo, pia iliripotiwa hivi majuzi kwamba Guimarães amenunua nyumba mpya kabisa kaskazini mashariki — kwa hivyo labda hana nia ya kuendelea hivi sasa.