Maafisa wa usalama Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamewatoroka wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushambulia kambi ya kijeshi.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawashikilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi Aprili.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB