Watu kumi wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ambapo vitongoji vimekumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha kunyesha usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, kulingana na shirika la habari la AFP likinuku polisi.
Jumla ya “watu 60,000, hasa wanawake na watoto”, “waliathiriwa pakubwa na mafuriko ya ghafla na mabaya ambayo yalikumba jiji hilo”, akulingana na polisi ya kenya katika taarifa yake, ikithibitisha kwamba Nairobi “iko ukingoni mwa janga la kibinadamu. Kupanda kwa maji kumeathiri vitongoji vya watu wenye maisha duni vyote viwili, kama vile Mathare, na vitongoji vingine vya watu wa hali ya juu, kama vile Runda ambapo makao makuu ya kanda ya Umoja wa Mataifa yanapatikana.
Kenya inaendelea kukumbwa na mvua kubwa inayonyesha Afrika Mashariki, ambapo msimu wa mvua unazidishwa na mfumo wa hali ya hewa unaoitwa El Niño. Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu (OCHA) liliripoti, kufikia Aprili 18, takriban watu 32 walifariki dunia na zaidi ya 40,000 kuhama makazi yao katika kaunti 21 kati ya 47 za nchi hiyo tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwezi Machi.
Jijini Nairobi, mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha ilisababisha mito ya Athi, Ngong na Mau Mau kuvunja kingo zake. Katika kitongoji cha watu wenye maisha duni cha Mathare, mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi, wakaazi walimezwa na maji hadi kiunoni, kulingana na picha zilizotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambalo lilikuwa likifanya shughuli za kuwahamisha kutoka eneo hilo.