Wizara ya afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema Alhamisi kuwa takriban watu 34,305 wameuawa katika eneo hilo wakati wa zaidi ya miezi sita ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.
Idadi hiyo inajumuisha takriban vifo 43 katika siku iliyopita, taarifa ya wizara hiyo ilisema, ikiongeza kuwa watu 77,293 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu vita vilipoanza wakati wapiganaji wa Hamas walipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba.
Viongozi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na zaidi ya nchi kumi na mbili walitoa taarifa ya pamoja Alhamisi kwa Hamas kuwaachilia mateka wengi ambao imekuwa ikiwashikilia huko Gaza kwa zaidi ya siku 200.
Habari hizo zilikuja wakati timu ya ulinzi wa raia wa Palestina ikitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza kile ilichosema ni uhalifu wa kivita katika hospitali moja ya kusini mwa Gaza, ikisema kuwa karibu miili 400 iliopolewa kutoka kwenye makaburi ya umati baada ya wanajeshi wa Israel kuondoka katika jengo hilo.