Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 leo Aprili 30, 2024 amesema :.
“Katika Mwaka 2023, jumla ya vibali 11,258 vya kuuza madini nje ya nchi vilitolewa ikilinganishwa na vibali 10,318 vilivyotolewa Mwaka 2022. Ongezeko la vibali hivyo kwa kiasi kikubwa limetokana na kuongezeka kwa uhitaji wa madini ya vito na makaa ya mawe nje ya nchi.
Aidha, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, jumla ya vibali 115 vya uingizaji madini nchini vilitolewa ikiwa ni hatua mojawapo ya kusimamia na kudhibiti biashara ya madini nchini.”- Mhe. Antony Mavunde, Waziri wa Madini
“Jitihada mbalimbali zimeendelea kufanyika kuhakikisha madini muhimu na madini mkakati yananufaisha Taifa. Jitihada hizo ni pamoja na kufanya tafiti na kutangaza fursa za uwepo wa madini nchini kupitia maono ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri”- Mhe. Antony Mavunde, Waziri wa Madini