Katika kuunga mkono makundi mbalimbali na kurudisha kwajamii, KCB Bank Tanzania imedhamini na kushiriki mbio fupi za hisani za Run4Autism Tanzania zenye lengo la kuongeza uelewa juu ya tatizo la usonji nchini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kama mgeni rasmi, alitoa pongezi za kwa Benki ya KCB Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono makundi jitihada mbalimbali kupitia uwekezaji kwa jamii.
Mkuu wa Idara ya Masoko, Uhusiano na Mawasiliano, Christina Manyenye akimuwakilisha Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, alisisitiza kuwa mbali na mafunzo ya ujuzi naufundi ya 2jiajiri, KCB Bank Tanzania itaendelea kutekelezaazma yake ya kuigusa jamii na makundi mbalimbali kwanamna tofauti.
“KCB Bank tunaungana na Lukiza Foundation katika kuletaelimu ili wazazi wengi wajitokeze na kuwasaidia Watoto wenye tatizo la usonji nchini, tunaamini kupitia mbio hizitunachangia katika kuleta mabadiliko Chanya kwa manufaaya jamii yetu, alisema.
Kupitia mbio hizi, benki imeonesha dhamira yake ya kuungamkono jitihada za kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa usonjina kuendeleza michezo nchini.
Mbali na hilo, benki ya KCB inashiriki katika masualambalimbali ya kimaendeleo ikiwamo kusaidia vijana kielimuna kiujuzi kupitia program ya 2jiajiri ambayo imekuwachachu katika kupunguza tatizo la ajira.