Mtoto wa gwiji wa Real Madrid, Marcelo, Enzo Alves, amesaini mkataba mpya na klabu hiyo hadi Juni 2027.
Enzo, 14, amekuwa akiichezea timu za akademi ya Madrid tangu 2017 na fowadi huyo mwenye sifa ya juu sasa anachezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 15. Ameweka kalamu kwenye karatasi juu ya kuongezwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania chini ya miaka 15, Enzo amefunga mabao 17 msimu huu.
Kijana huyo aliandika kwenye Instagram: “Nimefurahi kuendelea katika klabu bora zaidi duniani.”
Baba yake aliandika kwenye Instagram: “Hongera mwanangu kwa mafanikio mengine yaliyofikiwa. Furaha, kazi na uwajibikaji.”