WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma leo, Mei 6, 2024, ambapo ameliomba Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo ambayo ni zaidi ya shilingi trilioni 2.
Katika suala la Ujenzi, ukarabati viwanja vya ndege serikali imekwisha tenga bilioni 108.71.
“Ujenzi wa Kiwanja cha Arusha Shilingi bilioni 5.08, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Lindi Shilingi bilioni 13, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Moshi Shilingi bilioni 5, Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida Shilingi bilioni.
“Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Kiwanja cha Ndege cha Njombe kwa Daraja 4E. Shilingi milioni 692, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimataifa cha Serengeti Shilingi bilioni 1, Usanifu wa kina wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya TAA Shilingi milioni 400.
“Ujenzi wa Kiwanja cha Mwanza Shilingi bilioni 15, Ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba Shilingi bilioni 3.48, Ujenzi wa Kiwanja cha Mtwara Shilingi bilioni 7.3, Ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro Shilingi bilioni 50, Uboreshaji na Upanuzi wa Jengo la Pili la Abiria JNIA Shilingi bilioni 6.08,”