Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kusimamia makusanyo kupitia vyanzo mbalimbali vilivyo kwenye maeneo yao ili kuwezesha Serikali kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa Mei 6, 2014 na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Adolf Nduguru wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wakurugenzi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini nchi yanayofanyika kwenye Chuo cha Uongozi Mwl. Julius Nyerere kilichopo Kwa Mfipa – Kibaha mkoank Pwani.
Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi, Ndunguru amewasisitiza Wakurugenzi hao kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo ili pesa zinazotolewa na Serikali kwa kazi hiyo zilete tija kwa umma.
” Hakikisheni pesa zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo mnazipeleka mapema na kuzisimamia ili zifanye kazi kulingana na matakwa ya Serikali ili kuwaondolea wananchi changamoto” amesema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Sospiter Mtwale amesema Serikali imeona kuna umuhimu wa kuwapa mafunzo ya utendaji kazi wakurugenzi hao ikiamini kuwa wataongeza tija na ufanisi.