Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Bungeni Dodoma.
“Ili kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine na kuongeza fursa za elimu nchini Serikali itatekeleza yafuatayo:
“Serikali itatoa ufadhili kwa wanafunzi watano kutoka China wanaosoma lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam ili kubiasharisha lugha ya Kiswahili”
“Serikali itatoa ufadhili kwa wanafunzi watano raia wa Oman na wanafunzi watano raia wa Hungaria kusoma katika vyuo vikuu vya hapa nchini kulingana na mikataba”
– Serikali itashiriki katika mikutano ya Ushirikiano wa kikanda na kimataifa (inter-university council for East Africa- IUCEA, East African Community- EAC, Southern Africa Development Community- SADC, United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization – UNESCO na Africa Union – AU) ili kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa elimu ya juu” – Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda