Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amelaani tangazo la kampeni ya uchaguzi aliloliita la “uhaini” linaloonyesha kuchomwa kwa bendera ya nchi hiyo.
Tangazo hilo la mtandaoni na kwenye televisheni, ambalo lilizinduliwa mwishoni mwa juma na chama cha Democratic Alliance (DA), limezua taharuki katika mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni, huku baadhi ya Waafrika Kusini wakikiita chama hicho kuwa “kiziwi.”
Nchi hiyo itapiga kura katika uchaguzi wa wabunge Mei 29, katika kile ambacho kinatarajiwa kuwa kura nyingi zaidi tangu utawala wa kidemokrasia ulipoanzishwa mwishoni mwa ubaguzi wa rangi.
“Kuhusiana na kuchomwa kwa bendera, hata katika tangazo la kisiasa ambalo ni la uhaini,” Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari kaskazini mwa jimbo la Limpopo Jumanne.