Kocha wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique alisisitiza kuwa “anajivunia” timu yake licha ya kile alichokiita “kipigo kisicho cha haki” mikononi mwa Borussia Dortmund katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.
PSG ilikosa kutinga fainali mwezi ujao Uwanja wa Wembley baada ya kupoteza mechi ya Jumanne ya nusu fainali kwa 1-0 nyumbani na Wajerumani na kutoka kwa jumla ya mabao 2-0.
“Hisia zangu ni za huzuni. Haiwezi kuwa kitu kingine chochote. Hatukuweza kutimiza lengo letu,” Luis Enrique, ambaye aliiongoza Barcelona kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2015, aliwaambia wanahabari.
Alidokeza kuwa PSG walifunga bao hilo mara nne katika kipindi cha pili cha mchezo wa Jumanne, pia waligonga nguzo kwenye kipigo cha 1-0 wiki iliyopita katika mechi ya kwanza nchini Ujerumani.
“Sidhani tulikuwa duni kuliko sare. Tuligonga mbao mara sita. Jambo la kushangaza kuhusu soka ni kwamba wakati mwingine si sawa – tulipiga mashuti 31 na hatukufunga bao hata moja.
“Kandanda haikuwa sawa na sisi katika sare hii. Lazima tuikubali, tuipongeze timu iliyofika fainali, tuomboleze na kuondokana na masikitiko.”