Ukuaji wa kasi wa Teknolojia ya habari na mawasiliano na matumizi yake nchini Tanzania yamepelekea umuhimu wa sheria ya mtandao kukabiliana na makosa yatokanayo na matumizi ya mtandao kuwekwa kwa watumiaji hii ni kulinda miiko na sheria za mtu binafsi na hata wengine.
Utendaji makosa wa kwenye mtandao ni tofauti na makosa yanayofanyika na kusimamiwa na sheria nyingine.
Makosa ya mtandao siyo lazima yafanyike ndani ya mipaka ya kijiograa ya nchi husika na siyo lazima kitu kilichoibwa kihamishike Sheria zilizopo hazitambui makosa yanayofanyika kwenye mtandao hivyo kupelekea vyombo vya maamuzi kushindwa kutekeleza wajibu wake.
ili mtu adhibiwe kisheria ni lazima kosa liainishwe kwenye kanuni za adhabu au litambulike kisheria ndipo mtu anaweza kutiwa hatiani.
Kwa kutambua hilo Bunge la Jamhuri ya muungano lilipitisha sheria ya Makosa ya Mtandao tarehe 1 aprili 2015 na kuridhiwa na Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa tanzania tarehe 25 Aprili, 2015.
Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
Matumizi ya mitandao yote mikubwa kama Twitter, Instagram, JamiiForums, Facebook, Barua pepe, WhatsApp, blogu na data zote zilizo katika kifaa chochote cha kielektroniki yanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na sheria hii.
Vilevile sheria hii inawalinda wadau wote, wakiwemo wafanyabiashara dhidi ya usambazaji wa taarifa za uongo au taarifa zozote bila idhini ya mhusika na muhimu wake unakuja pale ambapo wapinzani wa kibiashara wakianza kuchafuliana sifa kwa ajili ya kuvutia wateja.
Hivyo basi kuepuka matumizi mabaya ya mtandao epuka kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao
Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao
Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)
Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii
Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu