Mafuriko katika Kaunti ya Tana River nchini Kenya yamezidisha tishio la ugonjwa wa kipindupindu, huku visa 44 vilivyoripotiwa vikiangazia wasiwasi kuhusu kuenea kwa magonjwa yanayotokana na maji.
Shirika la Afya Duniani (WHO) katika taarifa ya Jumanne, Mei 7 lilisisitiza juhudi za ushirikiano kati ya mamlaka ya Kenya, WHO, na mashirika mengine kufuatilia na kukabiliana na masuala ya afya ambayo yamezidishwa na mafuriko nchini kote.
“Visa 44 vya kipindupindu vimeripotiwa katika Kaunti ya Tana River, mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko. Serikali ya Kenya imeweka jibu la dharura la sekta nyingi, linaloongozwa na Kituo cha Operesheni za Dharura za Kenya katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi. ” Dkt Pius Mutuku, mtaalam wa magonjwa ya matibabu katika Wizara ya Afya alisema.
Alithibitisha athari za mafuriko hayo zimesababisha kufungwa kwa vituo 14 vya afya na uhaba wa mitambo mikubwa ya kutibu maji “na kusababisha uhaba wa maji ya kunywa kwa watu 3000”.