Milionea wa Ufaransa aliyekuwa mgonjwa mahututi alimwachia mfanyakazi wake wa Thailand urithi wa takribani Dola milioni 2.7 za Kimarekani sawa na Tsh Bill.7,006,500,000) katika siku yake ya kuzaliwa kabla ya kuripotiwa kujiua.
Baada ya taarifa hiyo tu urithi huo unasemekana ulisitishwa huku mamlaka ikichunguza iwapo mfanyakazi huyo anaweza kurithi kiasi hicho cha utajiri mara moja, gazeti la Bangkok Post liliripoti.
Bosi wa mfanyakazi huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 59 alikutwa amefariki hivi karibuni katika makazi yake katika kisiwa cha Koh Samui.
Hakuna taarifa zozote za mauaji, lakini uchunguzi unaendelea katika hoteli ya kifahari ya Catherine Delacote katika ufuo wa tambon Mae Nam kwenye kisiwa cha Koh Samui katika jimbo la Surat Thani.
Mwanamke huyo Mfaransa alikuwa ameacha mali ya jumla ya baht milioni 100( zaidi ya Bilioni 7 )kwa Nutwalai Pupongta, 49, mfanyakazi wake wa nyumbani kwa miaka 17.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hoteli hiyo ilijengwa kihalali. Lakini mamlaka bado haijaamua umiliki wa hisa katika kampuni inayomilikiwa na mwanamke Mfaransa aliyefariki dunia ambayo inamiliki hoteli hiyo.
Kampuni hiyo, GVNE, ilikuwa na wanahisa watatu. Delacote ilimiliki asilimia 4 ya hisa, huku watu wawili wa Thailand wakiwa na hisa zilizosalia.
Mwanamke huyo wa Ufaransa, ambaye alikuwa ametalikiana na mume wake Mfaransa, aligunduliwa amekufa karibu na bwawa la kuogelea ndani ya jumba la kifahari mnamo Aprili 29. Mwili wake ulikuwa na tundu la risasi na bunduki ilipatikana kwenye eneo la tukio.
Wenye mamlaka huko Koh Samui walisema kwamba msimamizi wa mirathi, akiwa na amri ya korti, anaweza kugawa mali ya marehemu mwanamke kulingana na wosia wake.
Rais wa Chama cha Utalii cha Koh Samui alisema kuwa idhini kutoka kwa wanahisa wawili wa Thai katika kampuni ya Catherine inaweza kuwa muhimu kwa uhamisho wa mali.
Zaidi ya hayo, wakili wa kisheria alibainisha kuwa ikiwa kampuni itamtumia mbia wakala kinyume cha sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani inaweza kupiga mnada mali yake.