Kati ya Jumatatu na Jumatano, Wapalestina 109 wameuawa na 296 kujeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema baadhi ya mashambulizi mabaya zaidi ya hivi majuzi yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel yalifanyika Rafah na kuua wanawake na watoto majumbani mwao:
-Wapalestina tisa, wakiwemo takriban watoto wanne na wanawake wawili, waliripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa wakati wanajeshi wa Israel walipolenga nyumba moja katika Kambi ya Wakimbizi ya Yebna, kusini mashariki mwa Rafah.
– Wapalestina tisa, wakiwemo watoto wanne na wanawake watatu, waliripotiwa kuuawa wakati nyumba moja ilipopigwa na wanajeshi wa Israel kwenye mtaa wa George mashariki mwa Rafah.
– Wapalestina wanne, wakiwemo watoto wawili na wanawake wawili, waliripotiwa kuuawa wakati wanajeshi wa Israel walipolenga nyumba moja katika kitongoji cha Al Junainah mashariki mwa Rafah.
– Takriban Wapalestina watano, akiwemo mwanamke na mtoto, waliripotiwa kuuawa wakati nyumba moja ilipopigwa na wanajeshi wa Israel katika kitongoji cha Al Barahma eneo la Tal As Sultan magharibi mwa Rafah.
– Wapalestina wanne, akiwemo mwanamke mmoja, waliripotiwa kuuawa wakati nyumba ilipolengwa na wanajeshi wa Israel katika mtaa wa Al Junainah mashariki mwa Rafah.
– Wapalestina wanne waliripotiwa kuuawa wakati vyumba viwili vilipopigwa na wanajeshi wa Israel katika eneo la Tal As Sultan magharibi mwa Rafah.