Mapema wiki hii, vyombo vya habari vya Indonesia viliripoti kisa cha ajabu cha mwanamume mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliishia kupiga simu polisi baada ya kugundua kuwa mwanamke ambaye alikuwa ameoana naye siku 12 tu kabla ys siku hiyo alikua kuwa mwanaume.
Mwanamume huyo inadaiwa alikutana na mchumba wake kwenye mtandao na baada ya kupendana, wawili hao waliamua kukutana ana kwa ana.
AK alikiri kwamba alimpenda mke wake mtarajiwa mara tu alipomwona kwa mara ya kwanza, na baada ya kukutana kwa ukarimu mara chache, alipata ujasiri wa kumtaka wachumbiane .
Mwanamume huyo anakiri kwamba mchumba wake alikuwa na tabia fulani, lakini hakuwahi kumshuku kuwa mwanamume aliyejificha.