Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi leo tarehe 09/05/2024 amewasili mkoani singida kwa ziara ya siku tatu akitokea mkoani Dodoma ambapo amepokelewa na viongozi wa chama,jumuiya na serikali katika kijiji cha Lusilile kata ya Kintinku halmashauri ya wilaya ya Manyoni ambapo baada ya kuwasili amepokea taarifa kutoka kwa viongozi mbalimbali wa mkoa wa Halmashauri ambapo wameeleza namna serikali inavyotoa fedha kwaajili ya utekeleza wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo hadi kufikia robo tatu ya mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya shilingi Bilion 9.1 zimepokelewa kutoka serikali kuu,wahisani na Mapato ya ndani sawa na aslimia 92% ya kiasi kilichoidhinishwa cha shilingi Bilioni 9.9 zikielekezwa katika miradi ya elimu,afya na ujenzi wa majengo mbalimbali pamoja na utekeleza wa shughuli za Tasaf.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji na kata hiyo waliojitokeza katika mapokezi hayo Hapi mbali na kutoa salamu za chama cha Mapinduzi amewahakikishi kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha maisha ya wananchi ndiyo maana inaendelea kutoa fedha za miradi yote inayoendelea kutekelezwa kila kona Nchini.
“serikali yenu ya chama cha mapinduzi ni serikali sikivu inayojali shida za watu ambao ndiyo wameiweka madarakani,ndiyo maana inatoa fedha nyingi kwaajili ya maendeleo hii ni kwasababu rais wetu anatupenda na anapenda maendeleo,niwaombe tuendelee kuiunga mkono kwa kushiriki katika kutekeleza miradi hiyo iliyopo katika maeneo yenu”alisema Rashid.
Awali Hapi amepokea taarifa ya Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Dkt Pius Chaya kuhusu changamoto ya uhaba wa maji katika kata ya Kintinku ambapo amemuomba katibu mkuu wa wazazi kuibeba changamoto ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa maji unaojengwa uweze kukamilika na kumaliza adha kwa wananchi ya kutafuta maji umbali mrefu jambo ambalo Hapi ameahidi kulifikisha kwa wahusika kukamilisha mradi huo.
Hapi anaendelea na ziara katika mkoa wa singida kwa lengo la kuimarisha jumuiya ya wazazi na kuimarisha chama cha mapinduzi CCM.