Ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambapo Mei 9, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2024/2025 Bungeni mkoani Dodoma.
Hizi ni nukuu zake alichozungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti hiyo.
‘Wizara kwa kushirikiana na maendeleo pamoja na sekta binafsi imepanga kutekeleza Jumla ya miradi 245 ya maji kwenye maeneo ya mijini.Baadhi ya miradi itakayoendelea kutekelezwa ni mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji Mto Kiwira kwenda Jiji la Mbeya’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu mradi Mto Rufiji kwenda mikoa ya Dar es Salaam na Lindi, na Mradi wa maji wa miji 28 Vilevile, Wizara imepanga kuendelea na Ujenzi wa miradi ya uondoshaji wa majitaka katika miji mikuu ya mikoa, miji mikuu ya Wilaya na miji midogo’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Wizara imepanga kuendelea kutekeleza Jumla ya miradi 1054 ya usambazaji maji vijijini katika maeneo mbalimbali.Aidha kwa akılı ambavyo havikafikiwa na huduma ya maji, Serikali imepanga kuchimba Visima vitano katika kila Jimbo la Uchaguzi kwenye maeneo ya vijijini na kwa kuanzia, Wizara itaanza Uchimbaji wa Visima 900’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Wizara itaendelea kubadili mitambo inayotumia Dizeli na kuweka Umeme wa Gridi ya Taifa au Nishati ya Jua ili kupunguza Gharama za uendeshaji wa skimu za maji; kuimaisha usimamizi wa mauzo ya maji na makusanyo kwenye CBWSOs kwa kufunga dira za Malipo kabla ya matumizi (Prepaid meters) kuweka mfumo wa pamoja wa utunzaji wa kumbukumbu za wateja na uandaji wa ankara (Unified Maji Biling System) na kujiunga kwenye mfumo wa makusanyo ya fedha za Umma (GePG)’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso