Wanyama wakali aina ya Viboko na Mamba wameendelea kuzua taharuki katika Halmashauri ya wilaya ya Geita hasa katika Maneno ya Kata ya Nkome, Kata ya Nyamboge pamoja na kata ya Butundwe ambapo Wananchi wamekuwa wakikamatwa na kuliwa na Wanyama hao ambao imekuwa kero kwa wananchi.
Hayo yameelezwa katika Kikao cha Robo tatu ya Mwaka wa 2023/2024 cha Balaza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Geita Baada ya Diwani wa kata ya Nyamboge Daud Msibakazahala kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Idala ya Maliasiri kuwa chukulia hatua Baada ya Mwananchi wake kuliwa na wanyama hao hivi karibuni.
Wakitolea ufafanuzi juu ya kero hiyo Baadhi ya Madiwani kutoka katika kata hizo akiwemo Diwani wa kata ya Nkome Masumbuko Sembe amesema hivi Majuzi mwananchi wake alikamatwa na wanyama hao na kupelekea kuuliwa jambo ambalo liliteta taharuki katika Maeneo yao huku wakiitaka idala ya Maliasiri kuchukulia suala hilo kwa unyeti zaidi.
Asaph Manya ni Afisa Maliasiri wilaya ya Geita amewataka Madiwani walio katika maeneo hatarishi kutoa taarifa hizo kwa Maafisa watendaji wa kata na vijiji na kutoa taarifa kwa mamlaka huska kwa ajili ya kuchanganua changamoto hizo kwani sheria zipo wazi endapo mnyama atahatarisha maisha ya watu huku akisema hajawai kupokea taarifa yoyote mbaya juu ya wanyama hao hatarishi.