Ikiwa ni siku ya pili Waziri wa Maji, Jumaa Aweso leo Mei 10, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2024/25 Bungeni mkoani Dodoma.
Hizi ni nukuu zake alichozungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti hiyo.
‘Kipande cha Nane chenye Mji wa Mafinga asilimia 17, Kipande cha Tisa Chenye Miji ya Rorya na Tarime asilimia 13 na Kipande cha kumi chenye anki wa Songea utekelezaji umefikia asilimia 3. kulingana na Mkataba mradi huo wa miji 28 unatarajiwa kukamilika katika Mwaka 2025/26’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Mradi wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi unatekelezwa kwenye Wilaya tano za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu katika Mkoa wa Simiyu.Mradi huo unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund- GCF) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 444.6’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Serikali imeendelea kuboresha huduma ya Usafi wa mazingira katika Maeneo mbalimbali ya mijini kwa kujenga miundombinu ya uondoshaji majitaka. Hadi mwezi April 2024, kilomita 39 za mtandao wa majitaka zimejengwa na idadi ya wateja waliounganishwa ni 1727’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Kanda ya Ziwa yote. Wizara inahakikisha mnapata majisafi salama na ya kutosheleza kutoka Ziwa Victoria .Wahenga walisema kula uhondo kwataka matendo, pasi matendo utakula uvundo.Mradi wa Butimba umedhihirisha kuwa kuwa nia Njema na Juhudi za Mama Samoa, Mwanza sasa mane delta kula Uhondo’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso