Michuano ya kombe la dunia leo imechukua sura nyingine kabisa baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Ujerumani.
Kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Belo Horizonte – Ujerumani wameweka historia ya mbili kubwa – kutinga fainali ya 8 ya kombe la dunia – hii ni mara nyingi kuliko timu zote duniani, pili kuifunga Brazil nyumbani kwao ikiwa ni mara ya kwanza kwa Brazil kupoteza mechi ya ushindani kwenye ardhi yao tangu mwaka 1975.
Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Muller, Toni Kroos mawili, Sami Khedira, Ander Schurrle nae akafunga mawili huku Oscar akiifungia Brazil goli moja la kufutia machozi katika mechi iliyoishwa kwa ushindi wa 7-1.
Ujerumani sasa anamsubiri mshindi wa kati ya Argentina vs Uholanzi hapo kesho ili kupata kujua mpinzani wake wa fainali itakayopigwa jumapili hii.