Siku ya Jumapili, Mei 12, hitilafu kubwa ya mtandao ilikumba sehemu za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, huku matatizo ya kebo chini ya bahari yakitajwa kuwa chanzo cha usumbufu huo ulioathiri mamilioni ya watu.
Nchi kama Kenya, Rwanda na Msumbiji na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na kukatika kwa mtandao.
Mashirika ya kimataifa ya mtandao yalisema kuwa hitilafu kwenye Mfumo wa Cable wa chini ya bahari wa Afrika Mashariki ulisababisha kukatika.
Kebo iliyoathiriwa iko kilomita 10,000 kwenye pwani ya mashariki ya Afrika yenye pointi tisa za kutua ikiwemo Sudan, Djibouti, Somalia, Kenya, Tanzania, Comoro, Madagascar, Msumbiji na Afrika Kusini.
Kampuni kuu za mawasiliano nchini Kenya Safaricom na Airtel, pamoja na MTN ya Uganda zilisema muunganisho wa intaneti utaathiriwa kwa sababu ya kukatwa kwa nyaya chini ya bahari.
Sasa, mtandao hufikiaje simu yako, kompyuta binafsi au kifaa mahiri kupitia kebo ya chini ya bahari?
Nyaya za chini ya bahari ni mabomba ambayo hubeba ishara kwa umbali mrefu kwa kasi ya juu sana kwa kutumia teknolojia ya mwanga.
Mabomba haya yanawekwa baharini ili kuunganisha mabara.
Ikizingatiwa kuwa seva nyingi za mtandao zimepangishwa Amerika Kaskazini, Ulaya au Asia, ili uweze kuzifikia, utahitaji muunganisho kati ya kifaa chako na seva.
Seva inarejelea kompyuta ambayo hufanya rasilimali kupatikana kwa watumiaji kupitia mtandao.
Kwa ufupi, kazi ya seva kuu ni kutumika kwa amri,
Kwa mfano, ikiwa unataka kufikia Gmail, utahitaji muunganisho kwa seva za Gmail, ambazo zinapangishwa nje ya nchi.
Bila muunganisho huo, hutoweza kupakia chochote kwenye ukurasa.