Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani mauaji na kujeruhiwa kwa maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza.
Kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la (ISNA), Farhan Haq, naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa, amesema katika mkutano wa waandishi wa habari kwamba Antonio Guterres amesikitishwa sana na mauaji na kujeruhiwa wafanyakazi wa afya wa Umoja wa Mataifa na kushambuliwa gari la umoja huo huko Rafah.
Farhan Haq ameongeza kusema kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anataka uchunguzi kamili ufanyike kuhusiana na shambulio lilifanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya timu za misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza.
Kulingana na vyanzo vya Palestina, wanajeshi wa Israel walipiga risasi gari lenye bendera ya Umoja wa Mataifa, na kuuwa mfanyakazi mmoja wa shirika hilo huko Rafah kusini mwa Gaza.
Itakumbukwa kuwa, wafanyakazi 7 wa shirika kutoa misaada la World Central Kitchen (WCK) waliuawa katika shambulio na jeshi la utawala ghasibu wa Israel kwenye eneo la Deir al-Balah katika Ukanda wa Gaza tarehe Mosi mwezi uliopita wa Aprili.
Tangu kuanza kwa mauaji ya kimbari yanayofanywahadi sasa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameshindwa kuchuku dhidi ya utawala haramu wa Israel kutokana na jinai zinazofanyika Ukanda wa Gaza kutokana na mashinikizo ya nchi za Marekani na nchi za Magharibi .
Baada ya kupita miezi saba tangu utawala huo bandia wa Kizayuni uvamie Ukanda wa Gaza bila kupata mafanikio yoyote Israei unazidi kuzama katika migogoro ya ndani na nje siku baada ya siku.
Katika kipindi chote cha zaidi ya miezi saba ya mauaji ya kimbari ya Gaza, utawala ghasibu wa Israel haujapata mafanikio yoyote zaidi ya kutenda jinai, mauaji, uharibifu wa majengo na hospital, jinai za kivita, ukiukaji wa sheria za kimataifa na kusababisha hali ngumu katika eneo hilo.