Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amesema Sekta ya Mawasiliano imeendelea kukua ambapo takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 62.3 Mwezi Aprili, 2023 hadi kufikia laini milioni 72.5 Mwezi Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 16.4.
Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2025 leo May 16,2024, Nape amesema “Watoa huduma wa Miundombinu ya Mawasiliano wamefikia 25 ukilinganisha na watoa huduma 23 Mwezi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 8.7”
tazama pia….