Ulimwenguni kote, harusi ni nyakati zinazohusisha furaha, lakini nchini India, ni maalum zaidi kwa sababu zote zinahusu mila na utamaduni na wakati mwingine, mila hizi zinaweza kuwa tofauti sana kwamba zinafanya vichwa vikubwa vya habari!
Katika wilaya ya Dakshina Kannada ya Karnataka, familia kutoka Puttur ilifanya hatua isiyo ya kawaida kwa kuweka tangazo katika gazeti la ndani tangazo hilo likimtafutia bwana harusi anayefaa ‘wa kiroho’ kwa binti yao, ambaye aliaga dunia miaka mitatu iliyopita.
Familia ilitafuta mchumba wa kudumisha mila inayoitwa ‘Kule Madime’ au ‘Pretha Maduve’.
Desturi hii ya zamani, ambayo inahusisha ndoa ya roho za wafu, inafanywa katika mikoa ya pwani ya Dakshina Kannada na Udupi.
Tangazo hilo linasomeka: “tunatafuta mchumba aliyefariki zaidi ya miaka 30 Tafadhali piga namba hiyo ili kupanga Pretha Maduve (ndoa ya mizimu).”
Familia hiyo, ikizungumza na gazeti la Times of India, ilifichua kwamba wamepokea karibu simu 50 kutoka kwa watu wanaopendezwa na wanaweza kuamua hivi karibuni tarehe ya kufanya sherehe hiyo.
Aidha walieleza kuwa wamekuwa wakimtafutia binti yao mchumba kwa miaka mitano iliyopita, kwa nia ya kudumisha mila ya ‘Kule Madime’.