Mpango wa mbunge wa jimbo la Nigeria wa kufadhili ndoa ya maharusi 100 walioachwa yatima kutokana na ghasia umezua mzozo kuhusu kanuni za kidini na kitamaduni na kutaka mahakama kuingilia kati.
Abdulmalik Sarkindaji, spika wa bunge la mtaa kaskazini-magharibi mwa Jimbo la Niger, alipanga kuunga mkono ndoa ya mayatima, ambao wote wamepoteza jamaa zao kutokana na mashambulizi dhidi ya vijiji na magenge yenye silaha kali.
Sarkindaji alisema alikuwa akiwasaidia tu wapiga kura wake, lakini waziri wa masuala ya wanawake na maafisa wengine wamekashifu pendekezo hilo.
Wameelezea wasiwasi wao kuwa baadhi ya yatima huenda wakawa na umri mdogo au kulazimishwa kufuata sheria ili kujinufaisha kifedha.
Harusi za watu wengi si jambo la kawaida nchini Nigeria, hasa katika maeneo ya kaskazini yenye Waislamu wengi, ambako zinaonekana kama njia ya kusaidia familia maskini kusimamia gharama zao.
Lakini ndoa za watoto wadogo pia hutokea katika maeneo ya vijijini ambako wanajamii wanatatizika na umaskini, ukosefu wa usalama na upatikanaji mdogo wa elimu.
Sarkindaji, mwanachama wa chama tawala cha All Progressive Congress, aliahidi wiki iliyopita kusaidia familia katika harusi hiyo kubwa baadaye mwezi huu.
Lakini siku ya Jumanne, Waziri wa Masuala ya Wanawake wa shirikisho Uju Kennedy-Ohanenye alitoa wito wa uchunguzi kuhusu umri wao, kibali chao cha ndoa na utambulisho wa wapenzi wao watarajiwa.