Fifa ilisema Ijumaa inataka wachezaji watumie ishara ya “mikono iliyopishana” kuwaashiria waamuzi wa matukio ya unyanyasaji wa kibaguzi, kwa kuwa inataka kukabiliana na ubaguzi katika mchezo huo.
Bodi ya shirikisho la soka duniani itafanya ubaguzi wa rangi kuwa kosa maalum katika kanuni za kinidhamu za wanachama wake wote 211, na adhabu “kali” ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa mechi.
“Msimamo wa kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi” katika kongamano la kila mwaka la Fifa huko Bangkok ulikuja baada ya miezi kadhaa ya mashauriano na wachezaji ambao wameteswa na wapinzani au mashabiki.
Nyota wa Real Madrid, Vinicius Junior amekuwa mmoja wa wachezaji wa hadhi ya juu waliozungumza kuhusu matusi mabaya anayokumbana nayo kwenye LaLiga.
Winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 23 amesema kuwa dhuluma za ubaguzi wa rangi alizopewa kwenye viwanja vya michezo nchini Uhispania zinapunguza hamu yake ya kucheza mchezo huo.