Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja mikoa sita iliyoripotiwa kuwa na idadi kubwa ya matukio ya wizi wa kimtandao ambayo ni Rukwa, Morogoro, Dar es Salaam, Tabora, Songwe na Mwanza.
Pia akasema kuwa takwimu zinaonesha laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 62.3 Aprili, 2023 hadi laini milioni 72.5 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 16.4.
Ameeleza kuwa watumiaji intaneti wameongezeka kutoka milioni 33.1 Aprili, 2023 hadi milioni 36.8 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 11.2.
“Watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 44.3 Aprili, 2023 hadi milioni 53 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 19.6,” amesema.
#keepiton#Beonline##digitalrightstz