Israel haikuhusika kwa vyovyote vile katika kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi na waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amir Abdollahian, afisa ameliambia shirika la habari la Reuters.
“Hatukuwa sisi,” alisema afisa huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina.
Dalili zote kwa sasa zinaonyesha kuwa helikopta hiyo ilianguka kwa sababu ya hali mbaya ya hewa na kutoonekana vizuri.
Iran na Israel ni maadui wa muda mrefu, na hawa wa mwisho wanapinga vikali mpango wa nyuklia wa Tehran.
Iran imeunga mkono, kufadhili na kutoa mafunzo kwa makundi kadhaa ya wakala katika eneo la Mashariki ya Kati kwa viwango tofauti, ikiwa ni pamoja na Hamas huko Gaza, Houthis nchini Yemen, Hezbollah nchini Lebanon na idadi ya makundi mengine yaliyoko Syria na Iraq.