Rais William Ruto wa Kenya anaanza ziara ya kihistoria nchini Marekani, ambayo inatarajiwa kuwa mapinduzi kwa Kenya yenye kulenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kwa kipindi cha miaka 15, ilifanyika na rais Daniel Arap Moi mwaka 1980 na Rais Mwai Kibaki mwaka 2003.
Inachukuliwa kama mfano mwema hasa ikizingatiwa kuwa mara ya mwisho ziara ya kiongozi wa Afrika ilifanyika mwaka 2009, wakati Rais George Bush alipokuwa mwenyeji wa rais John Kufour.
Rais anatarajiwa kuiwakilisha Kenya kama kitovu na eneo la kimkakati la uwekezaji.
Pia anatarajiwa kutoa hamasa kwa makampuni ya Marekani kuchukua fursa iliyopo na kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, alisema safari ya rais itaangazia ushirikiano wa miongo sita kati ya nchi hizo mbili na kuvutia ushirikiano zaidi.