“Rambirambi zetu kwa watu wa Iran kwa kifo cha Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian, na wengine walioangamia katika ajali ya helikopta,” Msemaji wa NATO Farah Dakhlallah aliandika kwenye akaunti yake ya X.
Rais wa Iran Ebrahim Raeisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian wameuawa shahidi katika ajali ya helikopta katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Azarbaijan Mashariki.
Helikopta iliyokuwa imembeba Rais Raisi na ujumbe alioandamana nao ilianguka Jumapili katika msitu wa Dizmar, ulioko kati ya miji ya Varzaqan na Jolfa katika Mkoa wa Azarbaijan Mashariki.
Rubani wa helikopta, rubani mwenza na wafanyakazi pia walikuwa miongoni mwa wengine waliokuwa kwenye chopa hiyo.
Rais Raisi na ujumbe alioandamana nao walikuwa wakirejea kutoka hafla ya kuzindua bwawa kwenye Mto Aras pamoja na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.