Siku chache baada ya kupokea taarifa ya kustaajabisha ya aliyekuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania (TMC), Joseph Bundala kujinyonga ndani ya choo cha ofisi aliyokua akiitumia ndani ya kanisa hilo.
Hatimaye mwili wa askofu huyo umezikwa kwenye Kanisa la Methodist lililopo eneo la Ihumwa ambalo ni miongoni mwa makanisa aliyoanzisha.
Askofu Bundala alikutwa amefariki dunia Mei 16, 2024 ,saa moja jioni ,akidaiwa kujinyonga kwa kutumia waya wa simu ndani ya choo cha ofisi yake, iliyopo kwenye kanisa la Methodist, Mtaa wa Ipagala A jijini Dodoma
Tumezungumza na Makamu Askofu mkuu wa kanisa hilo Samuel Nyanza amesema kutokana na tukio hilo lililotokea watalazimika kufunga kwa muda kanisa hilo na baada ya siku kadhaa itafanyika ibada ya utakaso na kulifungua upya kanisa hilo tena “kwasababu limetokea katika kanisa lile jambo kama hilo huwa tunafanmya kulisimamisha kulifunga lile kanisa kwa muda baada ya siku kadhaa kulingana na tamko ambalo mimi nalitoa kama kiongozi na utaratibu wa kanisa tutafanya ibada ya utakaso na kulifungua upya lile jengo tenandicho ambacho tumewaasa waumini”