Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemkashifu kwa hasira mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kutafuta hati ya kukamatwa kwake pamoja na viongozi wa Hamas kuhusu madai ya uhalifu wa kivita katika mzozo wa Gaza.
Netanyahu alisema alikataa kwa kuchukizwa na kwamba “Israel ya kidemokrasia” imelinganishwa na kile alichokiita “wauaji wa halaiki”.
Maoni ya Netanyahu yameungwa mkono na Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alisema hakuna usawa kati ya Israel na Hamas.
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Karim Khan, alisema kuna sababu za kuridhisha za kuamini kuwa Bw Netanyahu na Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant waliwajibika kwa uhalifu katika uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu huko Gaza.
ICC pia inatafuta kibali cha kukamatwa kwa kiongozi wa Hamas huko Gaza, Yahya Sinwar, kwa uhalifu wa kivita.