Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu Luhaga Mpina akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2024/25 amehoji misamaha ya kodi iliyowahi kutolewa kwa makampuni ya nje yameleta manufaa gani kwa Taifa.
Akichangia hoja hiyo Mpina amehoji ongezeko la bidhaa bandia nchini “Misamaha inayoombwa ikitumika vibaya nchi yetu inaweza kukosa kodi na kuwasaidia watu tu lakini inaweza ikatumika kama biashara tu kwamba ‘fanya hivi tukusamehe kodi’ ni mambo ambayo hayakubaliki lakini suala lingine ni serikali kufuta kodi kwa asilimia 15 katika utaratibu wa PVoC na mwaka jana wabunge tulilalamika kufutwa kwa utaratibu huo na leo Waziri ameshindwa kutueleza imepatikana tija gani katika kufuta utaratibu huo wa PVoC na tumefuta utaratibu huo TBS ikiwa haijajiandaa haina maabara ya kutosha matokeo yake nchi imekuwa na bidhaa feki” Luhaga Mpina