Kulingana na ripoti iliyotolewa Alhamisi ya WHO inasema watoto milioni 37 wenye umri wa miaka 13-15 wanatumia tumbaku kwa sababu biashara ya tumbaku ‘inalenga kikamilifu’ vijana.
Ripoti hiyo ilionya kwamba “katika nchi nyingi, kiwango cha matumizi ya sigara ya kielektroniki miongoni mwa vijana kinazidi kile cha watu wazima.”
Katika Kanda ya Ulaya ya WHO, 20% ya watoto wa miaka 15 waliohojiwa waliripoti kutumia sigara za kielektroniki katika siku 30 zilizopita, ilisema.
Haya yanajiri kabla ya Siku ya Dunia ya Kutotumia Tumbaku inayoadhimishwa tarehe 31 Mei, ambapo WHO inapaza sauti za vijana wanaotoa wito kwa serikali kuwalinda dhidi ya kuwa shabaha ya tasnia ya tumbaku na nikotini.
“Historia inajirudia, kwani tasnia ya tumbaku inajaribu kuuza nikotini moja kwa watoto wetu katika vifungashio tofauti,” alisema Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.
“Viwanda hivi vinalenga kikamilifu shule, watoto na vijana na bidhaa mpya ambazo ni mtego wenye ladha ya peremende jinsi gani wanaweza kuzungumza kuhusu kupunguza madhara wakati wanauza bidhaa hizi hatari na zinazolevya sana watoto?
Viwanda hivi vinaendelea kuuza bidhaa zao kwa vijana wenye ladha ya kuvutia kama peremende na matunda.
WHO inazitaka serikali kuwalinda vijana dhidi ya matumizi ya tumbaku, sigara za kielektroniki na bidhaa nyingine za nikotini kwa kupiga marufuku au kudhibiti vikali bidhaa hizo.
Mapendekezo ya WHO ni pamoja na kuunda maeneo ya ndani yasiyo na moshi kwa asilimia 100, kupiga marufuku sigara za kielektroniki zenye ladha, kupiga marufuku uuzaji, utangazaji na ukuzaji, ushuru wa juu, kuongeza ufahamu wa umma juu ya mbinu za udanganyifu zinazotumiwa na tasnia na kusaidia mipango ya elimu na uhamasishaji inayoongozwa na vijana. .