Katibu tawala mkoa wa Morogoro Dokta Mussa Ally Mussa amesema licha ya kukumbana na Changamoto mbalimbali lakini wamekua wakitoa huduma Bora Kwa wagonjwa ambapo amewataka kuepukana na vitendo viovu vinavyoweza kuwaharibika kazi ikiwemo rushwa ,dharau na ligha mbaya.
Dokta Mussa ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani ambapo kwa Mkoa Morogoro yamefanyika Morogoro mjini mkoani ikiambatana na kiapo ambacho wauguzi hawa wameapa Kwa lengo la kuwatumikia wananchi
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima , katibu tawala wa mkoa huo Mussa Ally Mussa pia amesema kuwa huduma nzuri za uuguzi huleta maendeleo na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambapo Serikali itaendelea kuwashika Mkono pia kwa kutambua umuhimu kazi hii.
Amesema Serikali inaendlea kutoa fedha Kwa ajili ya kujenga miradi kwenye sekta ya afya hivyo wananchi wanatakiwa kupata huduma Bora kama dhamira Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan.
Kwa Upande wake Mganga mkuuhospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dokta Kusirye Ukio amesema kuwa uuguzi ni kitengo Cha muhimu ambacho kinapaswa kulindwa,pia amewataka wauguzi hawa kuendelea kutekeleza majukumu yao kuwa uaminifu Ili kuleta chachu kwenye sekta ya afya
.
Hata hivyo amesema kuwa Hali ya malalamiko kutoka kwa wananchi sasa yamepungua licha uwepo wa baadhi wa wauguzi wakiendelea kutokwenda sahihi na amewataka kuhakikisha wanatoa huduma sahihi ili kumaliza malalamiko yote kwa wananchi ili ya upataji wa hudma Bora na uhakika
Akisoma risala ya wauguzi mbele ya Mgeni Rasmi Awadhi Juma Utime ambaye ni Katibu wa chama Cha wauguzi mkoa wa Morogoro amesema kuwa licha ya Changamoto wanazokumbananzo lakini wanafanya kazi ambapo kwa sasa mkoa wa Morogoro una takribani wauguzi 1737 hivyo wameiomba Serikali kusaidia kuongea wauguzi kwani kazi za uuguzi ambazo zilipaswa kufanywa na wauguzi 10 hufanywa na mtu 1
Kwa Upande wake mwenyekiti wa chama Cha wauguzi mkoa wa Morogoro Maria Mtweve amesema kuwa ili kuondoa changamoto zinazowakabili wauguzi wameiomba Serikali iwawezeshe kupata eneo kwaajiri ya kujenga ukumbi utakaowawezesha kujipatia kipatao kwaajiri ya kuendeleza Mfuko wa wauguzi
Maaadhimisho haya yamehudhuriwa na wauguzi kutoka sehemu mbalimbali Mkoani Morogoro huku yakiongozwa na kauli mbiu isemayo wauguzi sauti inayoongoza wekeza katika uuguzi,Heshimu,haki ,Linda afya.