Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya Tume ya Madini Mkoa wa Mbeya watoa mafunzo ya matumizi salama ya kemikali ya zebaki kwa Wachimbaji wadogo wa madini wa Kata ya Saza, Kijiji cha Patamela Wilaya ya Songwe Mkoa wa Mbeya.
Akizungumzia mafunzo hayo, Mhandisi wa Mazingira NEMC, Boniface Kyaruzi amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kupitia Mradi wa Kudhibiti Mtumizi ya kemikali ya Zebaki unaofadhiliwa na Bank ya Dunia na baraza hilo ambapo Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepewa jukumu la kutoa elimu kufuatia takwa la mkataba wa Minamata.
“Sambamba na hilo kufuatia Kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani isemayo, Urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa na Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame, tumewakumbusha wachimbaji wadogo kuhakikisha wanarejesha mazingira ya ardhi iliyoharibiwa kutikana na uchimbaji wa madini katika hali yake mara baada ya kumaliza shughuli za uchimbaji ili kuhakikisha ardhi inakua endelevu kwa matumizi mengine,”.