Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linaendelea kutumia mifumo ya Tehama katika kudhibiti makosa ya usalama Barabarani ambapo Jeshi hilo limebainisha kuwa kupitia mfumo huo mei 27 muda wa alfajiri limewabaini madereva watatu ambao wamevunja sheria za usalama Barabarani.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kinaendela kuboresha mifumo yake ambapo kwa sasa kitumia mfumo wa kufuatilia magari (VTS) katika kuwabaini madereva wanao wanaendesha magari mwendokasi.
SSP Zauda ameongeza kuwa kikosi hicho kinaendelea kutumia mifumo hiyo ili kuondoa malalamiko kwa watumiaji wa vyombo na wananchi kuhusiana na madereva wanavunja sheria za usalama barabarani huku akiweka wazi kuwa mapema leo tayari wamekamata madereva watatu waliozisha mwendo.
Aidha amesema kuwa kupitia mfumo huo umewasaidia katika kufuatilia madereva wakiwa maeneo tofauti tofauti ambapo alibainisha kuwa idadi kubwa ya madereva wanatumia vyombo vya moto hususani magari ya abiria wameendelea utii wa sheria bila shuruti huku akiwasihi kuwa kikosi hicho kinaendelea kuwafuatilia madereva wanao kikuka sheria kupitia mifumo hiyo.
Sambamba na hilo amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama Barabarani na wamiliki kuendelea kufanya marekebisho ya vyombo vyao kutokana na ongezo la abiria wengi hasa kipindi hiki ambacho wanafunzi wengi wamefunga shule kwa ajili ya mapumziko.
Kwa upande wake Apolinary Mwacha ambaye mweketi wa umoja wa madereva wa mabasi Mkoa wa Arusha licha ya kushukuru kupata nafasi ya kuona mfumo unavyo fanya kazi amesema kuwa utasaidia kupunguza mgongano baina ya askari na madereva huku amewaomba madereva wenzake kufuata sheria na taratibu za usalama Barabarani.