Jamii imetakiwa kuacha tabia ya ujenzi holela wa mkazi na badala yake watumia wataalamu kwaajili ya kupanga makazi yao nahivyo kuyapa dhamani maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Daktari dawa magembe ambaye ni muhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu aridhi wakati akizungumza na Millardayo.com katika maonesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea kufanyika jiji Tanga,na kusema kuwa ujenzi wa nyumba kiholela hupelekea adhari mbalimbali za mabadiliko ya tabia ya nchi kimazingira,kiuchumi na kijamii.
“Ujenzi holela unapelekea adhari nyingi za kimazingira kwani unasababisha kuleta madhara yanayo tokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani ujenzi holela unaenda kuziba maeneo alisi ya kupitisha maji lakini pili ujenzi holela unasababisha hatari ya moto kww magari kushindws kufika eneo la tukio lakini unadababisha maisha kuwa duni na kupeleke mali husika mfano nyumba hukosa dhamani”
Aidha Daktari dawa magembe alisema kuwa kwasada chuo hicho kina endelea na miradi mbalimbali ya upangazi wa matumizi bora ya aridhi ambapo kwa jiji la Tanga wanapanga fukwe ili iweze kufata kanuni za kimazingira na hivyo kuweza kutumika na watu wa rika zote na salama kwa ajili ya mapumziko.
Katika hatua nyengine alisema kuwa chuo hicho kinaendesha miradi mbalimbali kama mradi wa bomba la mafuta linalo lotoka uganda hadi chongoleani ambapo wame buni mradi wa makazi kwa kuzingatia kanuni za upangaji na uwepo wa bomba la mafuta.
Hata hivyo amesema kuwa miradi yote inayo buniwa hushirikisha viongozi mbalimbali wa halmashauri na hufanyika kialisia ili badaye iweze kutekelezwa na kuwasaidia wananch.