Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri serikali kuweka makato ya shilingi 50 kwa kila laini ya simu kwaajili ya mfuko wa Barabara(Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa Barabara nchini.
Kirumba ameshauri hilo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.
“tumekuwa tukisaini Barabara mpya kila kukicha Barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza road fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na Habari waliseama line ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila line shilingi 50 ili iweze kuisaidia Road Fundna hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje ‘Road Fund’ tunaisaidiaje” Mbunge Santiel Kirumba